COMPOSER | Edward Mote |
CHOIR | Sauti Tamu Melodies |
ALBUM | Nyimbo za Sifa |
CATEGORY | Ekaristia (Eucharist) |
Cha Kutumaini Sina Lyrics by Edward Mote
Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Damu yake na sadaka, nategemea daima
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake
Please Kindly drop a comment, Corrections and suggestions. Your Comment is a motivating factor for wikilyrics to perform greatly.